Leo Yatimizwa Lyrics

LEO YATIMIZWA

Leo yatimizwa maneno ya kale
Masihi kazaliwa, heko kwake
Isaya alisema Bikira atamzaa
(nasi) tufurahi na kumwimbia atokaye Mbinguni
Shangwe kuu tumpokeapo mgeni
Mwana wa Mungu Kristu
(tumshangilie) heko heko kwa bikira
Na mwanaye Yesu Kristu na tumshangilieni

  1. Herode upoe moto, usipayuke bure
    Yeye mfalme wa Mbinguni hana haja na wako
  2. Mwenye dhambi futa jasho takubebea mzigo
    Damu itafanya kazi, dhambi tatusamehe
Leo Yatimizwa
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
  • Comments