Leo Yesu Kazaliwa Lyrics

LEO YESU KAZALIWA

 1. Leo Yesu kazaliwa, wakristu twashangilia
  Habari njema kwa Wakristu, kokote washangilia
  Amezaliwa Mkombozi, atuokoe dhambini
  Mwokozi amezaliwa

  Njooni tumshangilie leo amezaliwa
  Aliyetabiriwa Mowokozi amezaliwa
  Ameacha enzi yake ili aje kutuokoa*2

 2. Malaika wa Mbinguni wanaimba aleluya
  Furaha kote duniani Wakristu wanashangilia
  Mwangaza kote duniani, Wakristu wameupata
  Mwokozi amezaliwa
 3. Azaliwe ndani yetu, ndilo tumaini letu
  Tukimwamini Yesu Kristu, azaliwe ndani yetu
  Tutaupata uzima alioleta uzima
  Mwokozi amezaliwa
Leo Yesu Kazaliwa
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
 • Comments