Ni Usiku Kweupe Lyrics

NI USIKU KWEUPE

 1. Ni usiku kweupe hapa kwani
  mwanga huu wa nini, kuangaza huku

  Msiche hayo mwende mbio wachunga
  Ni Masiha ashukiao
  Karibuni mtazameni mzaliwa
  Masiha hapo pangoni

 2. Twaarifu aliyelazwa chini
  Mwana Mungu yakini, Mfalme Mtukufu
 3. Sikieni ni malaika hao
  Kweli sauti yao, huko anagani
 4. Nyimbo gani zamtaja mwenye adhama
  Mleta kwetu salama, mshinda shetani
 5. Baadaye kila mwenye kutakata,
  Wokovu ni kupata kwa rehemaye
Ni Usiku Kweupe
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
SOURCETanzania
 • Comments