Uniokoe Uniokoe Lyrics

UNIOKOE UNIOKOE

Unioke uniokoe na watu hao wabaya
Na unikinge unikinge na wakatili
Wenye mawazo mabaya *2

 1. Daima hao huzusha ugomvi
  Na ndimi zao hatari kama nyoka
  Midomo yao maneno hatari
  Ni kama sumu hatari ya joka
  Mwenyezi Mungu naomba unilinde
  Kwa kucha zao wabaya na katili
 2. Wenye kiburi hutega
  Mipango yao waone uanguke
  Wametandaza kamba kama wavu
  Njiani wamezificha mitego
  Mipango yao yote wanikamate
  Sauti ya ombi langu sikiliza
 3. Mkombozi mkuu wangu umenikinga
  Salama hata wakati wa vita
  Waovu usiwape wanayotataka
  Mipango yao mibaya huivunje
  Wameinua kucha wamenizingira
  Uovu wao wenyewe uwapate
Uniokoe Uniokoe
CATEGORYTafakari
 • Comments