Kesheni Lyrics

KESHENI

 1. Kesheni pia ombeni, Mwokozi Yesu yuaja
  Vaeni mjifunge tayari tumlaki
  (Yesu) yuaja mawinguni, Wakristu tumlaki
  Kesheni . . .
 2. Upanga wako na uwe Neno la Bwana Yesu
  Na ngao na iwe na Mwana wa Mungu
  (Yesu) daima ukiwa naye hushindwi na maovu
  Upanga . . .
 3. Niumbie Roho mwema Bwana wangu
  Nishikie mkono ewe Masiha niwe wako milele
  (Yesu) nikuandame Masihi nisikuache kamwe
  Niumbie . . .
Kesheni
CATEGORYMajilio (Advent)
 • Comments