Hosanna Mwana wa Daudi Lyrics

HOSANNA MWANA WA DAUDI

@ (traditional)

Hosanna Mwana wa Daudi, ndiye mbarikiwa
Yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli
Hosanna juu Mbinguni
Enyi watu wote pigeni makofi
Mshangilieni Mungu kwa shangwe kubwa

 1. Kwa sababu Bwana aliye juu ni mwenye kutisha
  Ndiye mfalme mkuu wa dunia yote
 2. Atawatisha watu wa dunia chini yetu
  Na mataifa chini ya miguu yetu
 3. Atatuchagulia urithi wetu
  fahari ya Yakobo ambaye alimpenda
 4. Mwimbieni Mungu imbeni,
  Mwimbieni mfalme wetu mwimbieni
 5. Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote
  Imbeni kwa akili
 6. Mungu awamiliki mataifa
  Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu
 7. wakuu wa dunia wamekusanyika
  Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu
 8. Maana ngao za dunia zina Mungu
  Ametukuka sana
Hosanna Mwana wa Daudi
COMPOSER(traditional)
CATEGORYJumapili ya Matawi (Palm Sunday)
 • Comments