Ukarimu wa Bwana Yesu

Ukarimu wa Bwana Yesu
Alt TitleNani kama Bwana Yesu
Performed by-
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerStanslaus Mujwahuki
Views11,984

Ukarimu wa Bwana Yesu Lyrics

  1. Nani kati ya watala wote, wafalme wa dunia hii
    Aliyewahi kuandaa karamu, akaalika watu wote

    { Ni nani kama Bwana Yesu, mfalme wa mbingu na nchi
    Anayetualika sote kwenye karamu aliyoiandaa,
    bali tuwe na moyo safi } *2

  2. Sote tunaalikwa kushiriki, kwenye karamu yake Bwana,
    Tukiwa tajiri au masikini, bali tuwe na moyo safi.
  3. Ishara ya mapendo makubwa kwetu, kutoka kwake Bwana Yesu
    Kutoa mwili kutoa damu yake, kuzishibisha Roho zetu
  4. Ni fundisho kutoka kwake Bwana, tuuonyeshe ukarimu
    kwa ndugu rafiki au majirani, daima maishani mwetu