Nilikuomba Unipe

Nilikuomba Unipe
Performed by-
CategoryTafakari
Views2,244

Nilikuomba Unipe Lyrics

  1. Nilikuomba unipe (nipe) nguvu nipate kufanikiwa
    Nawe ukanipa udhaifu nipate kumnyenyekea Mungu
    Nilikuomba unipe (nipe) afya nitende mambo makubwa
    Nawe ukanipa maradhi nitende mambo mema zaidi

    Asante Mungu (twakushukuru) kwa wema wako wote
    Maana wewe u mwema, umenihurumia umenijalia mema yote
    Umeninyima yote (mabaya) ukanijalia yote (haya)
    Maana nayahitaji, umenihurumia umenijalia mema yote

    {Nasema ee Mungu - Na sasa ee Mungu wangu mpenzi
    Na sasa ee Mungu - Napenda kukiri neno hili moja
    Kati ya watu - Kati ya watu wa ulimwengu
    Nimebarikiwa - nimebarikiwa mno ee Mungu asante} *2

  2. Nilikuomba nipe utajiri nipate kujaa furaha
    Nawe ukanipa ufukara nipate kuishi kwa busara
    Nilikuomba nipe mamlaka wapate kunisifia
    Nawe ukanipa udhaifu nipate kumhitaji Mungu
  3. Nilikuomba nipe kila kitu nifurahie maisha
    Nawe ukanipa uhai nivifaidi vitu vyote
    Nilikuomba unipe na ujanja nionekane hodari
    Nawe ukanifanya mjinga nijifunze kumtii Mungu
  4. Nilikuomba nipe maarifa nipate kujulikana
    Nawe ukanifanya mnyonge nipate kumtumaini Mungu
    Nilikuomba unipe enzi nipate kumiliki nchi
    Nawe ukanitia majonzi nipate kumkimbilia Mungu