Mama Maria Mtakatifu

Mama Maria Mtakatifu
Performed by-
CategoryBikira Maria
Views5,851

Mama Maria Mtakatifu Lyrics

  1. Mama Maria Mtakatifu uliyechaguliwa na Mungu Baba
    Utuzalie Mkombozi atakayeokoa dunia nzima

    Ave Ave Ave Maria Ave
    Ave Ave Ave Maria Ave

  2. Mama Maria utuombee na sala zetu zifike kwa Mwanao
    Utuongoze kwa sala tusipotoshwe na mwovu ibilisi
  3. Mama Maria tusaidie tuwe na nguvu katika sala zetu
    Sala zetu zituwezeshe, kufika Mbinguni kwa muumba wetu
  4. Mama Maria utupatie msaada wako katika uchungu wetu
    Utulinde utuongoze ili tuweze kufika juu Mbinguni