Macho Yetu Hukuelekea

Macho Yetu Hukuelekea
Performed by-
AlbumUwe Nasi Mama Maria
CategoryBikira Maria
Views3,344

Macho Yetu Hukuelekea Lyrics

  1. Macho yetu yamekuelekea wewe Mama Maria
    Ndiwe mwombezi wetu
    Mama bora mwenye huruma na unyenyekevu wa moyo
    U kimbilio letu

    Utuombee maria, sisi wanao, ili tusije kupotea
    Utawala wa shetani umetuzunguka, maisha yetu ya mashaka
    Utusimamie mama maisha yetu yote tufike kwake Baba

  2. Vishawishi vyake shetani vinatusonga siku zote
    Uovu umezidi
    Utuombee kwake Baba atupe ujasiri mwingi
    Tushinde mjaribu
  3. Tunapenda kuwatendea watu wotee yaliyo mema
    lakini tunashindwa
    Ukivunje kiburi kilichomo ndani ya nyoyo zetu
    Tuwe wema daima