Nimeingia Mahali Hapa Lyrics

NIMEINGIA MAHALI HAPA

@ E. I. Kalluh

Nimeingia mahali hapa patakatifu,
kuja kumwabudu Bwana
{Amani na iwe ndani ya ngome zako
Na salama ndani ya nyua zako } *2

 1. Makao yako yapendeza sana,
  Ee Bwana Mungu wa majeshi
  Nakipenda kikao cha nyumba yako
  Na mahali pa hema ya utukufu wako
 2. Nalifurahi waliponiambia
  Tutaingia nyumbani kwa Bwana
  Sasa miguu yetu imesimama
  Katika milango yako ee Yerusalemu
 3. Ee Mungu wangu
  Muumba wangu
  Kuwe furaha yangu
  Nikutumikie kwa moyo mkunjufu mimi mwanao
Nimeingia Mahali Hapa
COMPOSERE. I. Kalluh
CATEGORYEntrance / Mwanzo
SOURCETanzania
 • Comments