Mchaka Mchaka Twendeni Mbio Mbio Lyrics

MCHAKA MCHAKA TWENDENI MBIO MBIO

@ Victor Aloyce Murishiwa

 1. La mgambo sasa limelia tembea ndugu yangu tena ukaze mwendo
  Safari yetu bado ni ndefu tushikane tutembee pamoja
  Milima pia nayo mabonde, tazama visije kuwa ni vikwazo kwako
  Ubebapo Neno lake Mungu songa mbele usirudi nyuma

  {Hima hima twendeni kwa pamoja
  Mchaka mchaka twendeni mbio mbio
  aee iye ye he he he hehe
  aee iye ye he he he iye
  Twendeni wote mbinguni kwa Baba} *2

 2. Watu wengi wana mali nyingi lakini kutoa sadaka kwao ni ndoto
  Wengi wao bila kuogopa humpa Mungu wao chenji
  Wengine huwatesa wajane jamani tena kuwanyanyapaa yatima
  Ikiwa unaitamani mbingu tenda wema na twende pamoja
 3. Tuzingatie tabia yako nao wale wenzetu pia tuwasaidie
  Badala ya kusubiri wafe na kutazama kwenye misiba
  Kumbukeni maneno ya Yesu aliyonena kupitia Injili Luka
  Mimi nilipokuwa mgonjwa hamkuja kunitazama
 4. Wengine wamekataa toba husema siwezi kutubu kwa mwanadamu
  Wamesahau ya kwamba Mungu alituachia makasisi
  Amewapatia mamlaka hakika watakalolifunga duniani
  Na mbinguni pia itafungwa ole wenu mnaowadharau
Mchaka Mchaka Twendeni Mbio Mbio
COMPOSERVictor Aloyce Murishiwa
CATEGORYTafakari
SOURCETanzania
 • Comments