Mpenzi wa Yesu

Mpenzi wa Yesu
Performed by-
AlbumBikira Maria
CategoryWatakatifu
Views2,263

Mpenzi wa Yesu Lyrics

  1. Mpenzi wa Yesu tusaidie ,
    Mama Theresia tusimamie *2

  2. Ewe Theresia Mtakatifu
    Twakujia wewe mwaminifu
    Jionyeshe kwetu sisi wanao
    Tusaidie kwa neema za Mungu
  3. Ewe Theresia duniani humu,
    Umeishi kwa unyenyekevu
    Tufanyayo twayatolea kwako
    Yakoleze yawe kama yako
  4. Uliteseka mateso mengi sana
    Kwa ajili ya Yesu mpenzio
    Tusaidie kukubali mateso
    Tuwe nasi wapenzi wa Yesu
  5. Ulitumwa kuwafundisha watu
    Njia Ndogo kumwendea Yesu
    Nasi utufundishe Njia yako
    Tuzifuase fadhila zako
  6. Mama Theresia mataifa yote
    Wewe Mlinzi Msimamizi
    Fukuza giza lote mioyoni
    Tunyeshee yako mawaridi
  7. Theresia mwema tusaidie ,
    Saa ya kufa kwetu ikiwadia ,
    Ili nasi tuseme kama wewe ,
    Ee mungu wangu ninakupenda