Kwa Jinsi Ujionavyo Lyrics

KWA JINSI UJIONAVYO

@ J. Urassa

Kwa jinsi ujionavyo (ndivyo) ndivyo ulivyoumbwa
Tena kwa mfano wake Yesu Kristu Mwokozi wetu
Furaha leo tuimbe shangwe
Tupige ngoma filimbi na vigelegele
Tufurahi tufurahi na Bwana Yesu

 1. Yeye mwenyewe aliona kwa jinsi hii utapendeza
  Sasa mbona wewe wamsahau Bwana Mungu wako
  Waisahau hata Sabato siku ya kumshukuru Mungu
 2. Tusijiongeze vitu vingine ndugu vya kujipamba
  Njoo kwake Bwana Yesu atakupamba upendeze
  Ili uweze kufika kwake Mungu kwenye uzima milele
 3. Ni Yesu Kristu peke yake aliye na upendo zaidi
  Katuandalia karamu kabla ya mauti yake
  Kaibariki kila tuilapo tupate uzima milele
 4. Ulapo bila kustahili ndugu ungoje hukumu yako
  Alisema mwenye moyo safi ajongee mezani
  Siku ile ya hukumu nitamwita kwenye ufalme Mbinguni
Kwa Jinsi Ujionavyo
COMPOSERJ. Urassa
CHOIRSt. Cecilia Kijenge
CATEGORYTafakari
SOURCETanzania
 • Comments