Nyumbani Mwake Bwana Lyrics

NYUMBANI MWAKE BWANA

Nyumbani mwake Bwana tuingie kwa furaha.
Twendeni tumwabudu tunjongee mbele zake. *2

 1. Njoni tumsujudu yeye aliyetuumba
  Yeye anatawala kwa haki na uamini.
 2. Yeye ni Mungu mwenye utukufu wa ajabu
  Yeye ni Mungu mwenye radhi nyingi na rehema.
 3. Bwana ni mtawala amejaa utukufu na mashuhuda
  Yake yastahili imani.
 4. Yeye ni Mungu wetu wa amani na mapendo
  Yeye ni Mungu mwenye utukufu wa ajabu.
 5. Tumpigie shangwe mwamba wa wokovu wetu
  Ni Mungu wa ujuzi na ni Mungu wa fahamu.
 6. Na kwa nyimbo za sifa tujongee uso wake
  Vifijo na nderemo tumsifu Mungu wetu
 7. Na enyi waadili tukuzeni jina lake
  Mfanyieni shangwe yeye aliyetuumba.
Nyumbani Mwake Bwana
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments