Ndiwe Sitara Yangu Lyrics

NDIWE SITARA YANGU

@ D. E. Ng

{Ndiwe sitara yangu Bwana
Utanihifadhi na mateso
Utanizungusha nyimbo za wokovu
Nyimbo za wokovu } *2

 1. Nalia mchana kutwa, nalia usiku kucha
  Lakini nafuu sipati Bwana usinitupe
 2. Bwana ni mdudu, wala si mtu kabisa
  Nimepuuzwa na kudharauliwa na kila mtu
 3. Ulimi wangu wang'ata kinywani mwangu ee Bwana
  Umeniacha kama mpumbavu mimi ninaangamia
 4. Bwana wewe ulitoa, Bwana wewe umetwaa
  Nichukue nami nikapumzike pema peponi
 5. Atukuzwe Mungu Baba, na mwanaye mtukuka
  Atukuzwe na Roho Mtakatifu milele amina
Ndiwe Sitara Yangu
COMPOSERD. E. Ng
CHOIRSt. Kizito Makuburi
CATEGORYZaburi
SOURCEDar-es-Salaam Tanzania
 • Comments