Nirudieni Mimi
| Nirudieni Mimi | |
|---|---|
| Alt Title | Lakini Hata Sasa |
| Performed by | Malaika Mkuu Mikaeli Chang'ombe |
| Album | Mwanga wa Mataifa |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | Aloyce Goden |
| Views | 79,188 |
Nirudieni Mimi Lyrics
{Lakini hata sasa, asema Bwana
Nirudieni mimi, kwa mioyo yenu yote } *2- Fanyeni mabadiliko mioyoni mwenu
Kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza
Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote - Pigeni tarumbeta huko Sayuni
Wambieni watu wote ili wafunge
Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote - Kusanyeni watu wote waleteni kwangu
Waleteni na watoto hata na wazee
Nirudieni Mimi kwa mioyo yenu yote - Mpingeni yule mwovu atawakimbia
Nikaribieni nami nitawakaribia
Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote - Takaseni mikono yenu iliyojaa dhambi
Safisheni mioyo yenu yenye nia mbili
Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote