Nimtumikie Nani

Nimtumikie Nani
Performed by-
AlbumRamani ya Mbinguni
CategoryTBA
ComposerC. A. L. Ndomelo
Views1,864

Nimtumikie Nani Lyrics

  1. Nimtumikie nani zaidi ya Mungu, aliyeniumba
    Hakuna aliye sawa na Mungu, nimtumikie nani mimi
    Pumzi ya uhai wangu, yatoka kwake, nimwogope nani mimi
    Hakuna aliye sawa na Mungu, nimtumikie nani mimi
    Hakuna oo tena hakuna mwingine,
    nitamtumikia Mungu aliyeniumba milele

  2. Naamini hakuna aliye sawa naye Mungu
    Lolote apendalo yeye Mwenyezi hutimia
    (Tena) hakuna awezaye kumpinga akipenda
  3. Naamini hakuna aliye sawa naye Mungu
    Aliyeumba nchi bahari milima na wanyama
    (Tena) akaniumba mwanadamu nivitawale vyote
  4. Naamini hakuna aliye sawa naye Mungu
    Aliyenitoa toka hutumwani mwa shetani
    (Tena) akanipigania ona sasa niko huru