Alidharauliwa na Kukataliwa Lyrics

ALIDHARAULIWA NA KUKATALIWA

@ Martin M. Munywoki

Alidharauliwa na kukataliwa kukataliwa na watu
Mtu mwenye huzuni nyingi ajuaye sikitiko sikitiko

 1. Kwa maana alikua kama mche mwororo
  Na kama mzizi katika nchi nchi kavu
  Yeye hana umbo hana umbo wala uzuri
  Hata tumwonapo tumtamani
  Kama ambaye watu humficha nyuso zao
  Wala hatukumhesabu yeye kuwa kitu
 2. Hakika amechukua masikitiko yetu
  Amejitwika huzuni zetu amejitwika
  Lakini tulimdhania kuwa amepigwa
  Amepigwa na Mungu na kuteswa
  Bali alijeruhiwa kwa ma-kosa yetu
  Alichubuliwa kwa maovu maovu yetu
 3. Adhabu ya amani yetu kawa juu yake
  Na kwa kupigwa kwake yeye sisi tumepona
  Sisi sote kama kondoo tumepotea
  Kila mmoja njia yake mwenyewe
  Bwana ameweka juu yake maovu yetu
  Alionewa laki-ni alinyenyekea
 4. Kaonewa wala hakufunua kinywa chake
  Kama mwanakondoo akipelekwa machinjoni
  Kwa kuonewa kuhukumiwa kaondolewa
  Ni nani atasimulia haya
  Maana amekataliwa mbali nayo nchi
  Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya
 5. Ingawa hakutenda jeuri kinywani mwake
  Lakini Bwana aliridhika kumchubua
  Utakapofanya nafsiye dhabihu kwa dhambi
  Ataona uzao wake yeye
  Ataishi siku nyingi na mapenzi ya Bwana
  Yatafanikiwa mkononi mkononi mwake
Alidharauliwa na Kukataliwa
COMPOSERMartin M. Munywoki
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
REFIsaiah 53
MUSIC KEYB Flat Major
TIME SIGNATURE4
4
NOTES Open PDF
 • Comments