Misa ya Mtakatifu Veronika

Misa ya Mtakatifu Veronika
Performed by-
CategoryMisa (Sung Mass)
ComposerMartin M. Munywoki
Views4,849

Misa ya Mtakatifu Veronika Lyrics

EE BWANA UTUHURUMIE

  1. Ee Bwana (Bwana Mungu) utuhurumie (ee Bwana)
    ee Bwana Mungu (tuhurumie) utuhurumie (ee Bwana ee Mungu Mungu utuhurumie
  2. Ee Yesu (Kristu) utuhurumie
    Ee Yesu Kristu utuhurumie

UTUKUFU

  1. Utukufu (juu) kwa Mungu Mbinguni
    Na amani iwe kote duniani (tunakuabudu)


    Tunakusifu Bwana twakuheshimu Bwana tunakuabudu
    Twakutukuza Bwana twakuheshimu Bwana
  2. Ewe Bwana Mungu Baba mfalme wa Mbinguni
    Tunakushukuru kwa utukufu mkuu, Mungu Baba Mwenyezi
  3. Ewe Bwana Yesu Kristu Mwana wa pekee
    Mwana kondoo Mungu uondoaye dhambi, utuhurumi-e
  4. Uondoaye dhambi zetu utusikie,
    Ewe uketiye kuume kwa Mungu Baba, utuhurumi-e
  5. U pekee Bwana Mtakatifu na u Kristu
    Pamoja naye Roho katika utukufu, wake Mungu milele

ALELUYA

  • Aleluya (aleluya) aleluya (aleluya) aleluya aleluya

NASADIKI

  1. Nasadiki (kwa Mungu Baba),
    nasadiki (kwa Mungu Mwana)
    Nasadiki (kwa Mungu Roho) nasadiki

  2. Nasadiki kwa Mungu mmoja Baba ye-tu Mwenye-zi
    Nasadiki Yesu Kristu mwana wake wa pekee
    Nasadiki alipata mwili kwa Roho Mtakati-fu
    Nasadiki kazaliwa na Bikira Maria
  3. Aliteswa alisulubiwa kwa amri ya Pnsyo Pilato
    Akafa na akazikwa na kushuka kwa wafu
    Alifufuka siku ya tatu na kupaa juu Mbingu-ni
    Toka huko tarudi kuhukumu ulimwengu
  4. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu na Kanisa Katoliki
    Nasadiki Ushirika wao Watakatifu
    Nasadiki ufufuko wa miili na ondoleo la dhambi
    Nasadiki uzima wa milele na milele

MTAKATIFU

  • Mtakatifu (Bwana Mungu) Mtakatifu (wa Majeshi) *2
    Mbingu na dunia zimejaa zimejaa
    Zimejaa utukufu wako Bwana
  • {Hosanna juu Mbinguni Hosanna Mbinguni juu Hosanna juu } *2
    Amebarikiwa amebarikiwa yeye
    Yeye ajaye kwa jina lake Bwana

FUMBO LA IMANI

  • Yesu Kristu alikufa Yesu alifufuka
    Atarudi Yesu atakuja tena

AMINA

  • Amina (amina) amina (amina) amina amina

BABA YETU

  1. Baba Yetu uliye Mbinguni, jina lako litukuzwe daima
    Na ufalme wako na ufike na mapenzi yako yatimilike

    Utakalo (utakalo) lifanyike (lifanyike) duniani (duniani) kama Mbinguni *2

  2. Tupe leo na mkate wetu tupe mkate wetu wa kila siku
    Tusamehe na makosa yetu vile tusameheavyo wengine
  3. Situtie vishawishini bali utuopoe maovuni
    Situtie vishawishini bali utuopoe maovuni
  4. Kwa maana ufalme ni wako na nguvu pia nao utukufu
    Kwa maana ufalme ni wako na nguvu pia nao utukufu

MWANA KONDOO WA MUNGU

  1. Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
    Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
    Tuhurumie (tuhurumie) utuhurumie
  2. Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
    Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
    Tuhurumie (tuhurumie) utuhurumie
  3. Ee Mwana Kondoo wa Mungu,
    Unayeziondoa dhambi za dunia (dhambi zote za dunia)
    Tupe amani (tupe amani) utupe amani