Watikisa Kibuyu Lyrics

WATIKISA KIBUYU

@ E. A. Minja

Nini siri ya moyo wako kupenda kuwa mtu wa roho mbaya?
Daima moyo wako wasononeka kwa kujiuliza kwa nini?
Jirani yako anapofanikiwa moyo wako wakosa raha
Si zuri si jema moyo wako wakutesa ukiwaza kwa nini!

Na tazama sasa- unachokifanya,
Ni kukimbilia - kutikisa kibuyu
Na imani yako - ni kwenye kibuyu na kibuyu ndiye mungu wako

 1. Wengine wanakiita ni kinga na kukifanya kama mungu wao
  Na tena jina jingine ni 'kimo' sababu yake na kiza ni wivu
  Unajisifia ni mtu mwema mwenye roho iliyo na huruma
  Lakini kwa ndani wewe mbaya roho imetawaliwa na wivu!
  Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu!
  Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu!
 2. Mtoto wa jirani kafaulu katika kazi au ni masomo
  Ukijua wakiwaza kibuyu ugeuze miguu yake nyuma
  Wenzako wanaongeza bidii ya kujituma kwenye kazi zao
  Wewe unawatazama vibaya na kuanza kukiwaza kibuyu
  Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu
  Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu
 3. Unapomtazama ndugu yako kajenga nyumba na inapendeza
  Ukiitazama moyo wauma sasa wawaza huyu asiishi!
  Ukirudi kazi kwako ni moja kukitikisa tikisa kibuyu!
  Ah! kumbe waroga umejawa na imani chafu!
 4. Sasa jifikirie ndugu wewe badili roho yako yenye wivu
  Na kuutengeneza moyo wako ukafanane nao malaika
  Ukirudi kazi kwako ni moja ni kupiga magoti na kusali
  Ah! Kumbe waomba upendo uwepo duniani
Watikisa Kibuyu
COMPOSERE. A. Minja
CHOIRSame KMJ
ALBUMWatikisa Kibuyu
CATEGORYTafakari
 • Comments