Sauti za Kuimba Lyrics

SAUTI ZA KUIMBA

@ Martin M. Munywoki

Sauti za kuimba ni talanta zawadi (Tumepewa ) na Mungu tumwimbie } *2
Haya basi nyanyukeni tumsifu
{Ninyi waimbaji (pazeni) zipaazeni sauti (hubirini) kwa sauti zenu } *2

 1. Mwimbieni Bwana kwa ala za muziki zote zenye sauti tamu
  Mpigieni ngoma na baragumu
  Aee za muziki zote zenye sauti tamu
  Mpigieni ngoma na baragumu
 2. Jongeeni enyi watunzi wachezaji wa vinanda na waimbaji
  Jiungeni nasi sifiche vipaji
  Aee wachezaji wa vinanda na waimbaji
  Jiungeni nasi sifiche vipaji
 3. Sauti ya kwanza na pili wapendeza wanapoimba pamoja na
  Na sauti ya tatu na nne ona
  Aee wapendeza wanapoimba pamoja na
  Na sauti ya tatu na nne ona
 4. Kusifu kwapendeza sana duniani pia mbinguni ni furaha
  Haya msifuni kuimba ni raha
  Aee duniani pia mbinguni ni furaha
  Haya msifuni kuimba ni raha
 5. Kuimba huondoa dhiki ni faraja kwa waliokata tamaa
  Ama burudani kwa walozubaa
  Aee ni faraja kwa waliokata tamaa
  Ama burudani kwa walozubaa
 6. Sauti zenu ni talanta amueni jinsi mtazi-tumia
  Angalieni mimi ninamwimbia
  Aee amueni jinsi mtazi-tumia
  Angalieni mimi ninamwimbia
Sauti za Kuimba
COMPOSERMartin M. Munywoki
CATEGORYUtume wa Uimbaji
 • Comments