Nitumwe Mimi Lyrics

NITUMWE MIMI

@ Bernard Mukasa

   // utangulizi //

   Hayo mliyofunuliwa, bila kuyalipia kitu, (nayo) ndiyo,
   Yale mliyotumwa, kwenda kwa walio wadogo
   Mungu alowatunukia awe mkuu pekee yake
   (Jiulize) nani kwenu (aliyeomba) kuzaliwa!
   (Jiulize tena) nani kwenu (anaijua) siku ya kufa!
   Hakuna! Hakuna! ha!

   // kiitikio //

Hakuna jambo mnalomiliki hapa duniani
Yote mliyo nayo yana mwenyewe mnamjua
Naye amewapa haya kusudi mtumikiane
Ili kusiwepo na matabaka miongoni mwenu
Hiyo ndiyo hekima - ee aa ee
[b:] Hiyo ni hekima ni hekima tele
Hiyo ndiyo hekima -ee aa ee
Ndugu hiyo ndiyo hekima ya kweli

// mashairi //

 1. Kama mliyo nayo yote yangekuwa yenu
  Hiyo pumzi mnayojivunia wapendwa,
  Isingekuwa inakiogopa kichomi
  Ingeendele-a hata palipo kichomi!
 2. Uzuri wa sura zenu zenye ngozi laini
  Inakuwaje hamuwezi kuelekeza,
  Usiungue hata kwenye maji ya moto
  Na usioze unapolala kaburini!
 3. Elimu na vyeo vyenu na mamlaka yenu
  Akili nyingi ufundi navyo vipaji vyenu,
  Mbona hamvitumii mkiwa usingizini
  Na mnaota ndoto sawa na za watoto!

  // hitimisho //

  Basi mimi, ninahimizwa, kujiepusha, kujiinua
  Nijishushe mbele ya wote, wawe wakubwa au wadogo
  Nisijiinue kati ya watu hata siku moja,
  Badala yake nijinyenyekeze ili nifikike,
  Akihitajika atakayewatumikia watu
  Nijitokeze kwa haraka ili wanitume mimi, daima

  Nijitokeze kusudi wanitume mimi
  Nijitokeze, kuitikia wito daima
  Nijitokeze kusudi wanitume mimi
  Na nikitumwa niwe mwaminifu daima
  Nijitokeze kusudi wanitume mimi
  Nijitokeze wanitume na Mungu atukuzwe daima
  Nijitokeze kusudi wanitume mimi

  Nijitokeze, nijitokeze leo
  Nijitokeze kusudi wanitume mimi
  Nijitokeze, nijitokeze daima
  Nijitokeze kusudi wanitumie mimi, milele!
Nitumwe Mimi
ALT TITLEKidole Juu
COMPOSERBernard Mukasa
CATEGORYTafakari
SOURCETanzania
 • Comments