Tuvumiliane

Tuvumiliane
Performed by-
CategoryTafakari
ComposerMartin M. Munywoki
Views2,650

Tuvumiliane Lyrics

  1. Tuvumiliane tuvumiliane, tuishi kwa upendo nao wenzetu
    Tuwakubali hao jinsi walivyo, ijapokuwa hawafanani nasi

  2. Wapo walio masikini wahitaji, miongoni mwetu
    Tusiwachoke wanapoombaomba, tuwavumilie
    Wengine hawana elimu kama sisi, miongoni mwetu
    Tuwaeleze kwa upole na pia, tuwavumilie hivyo
  3. Wengine wa asili tofauti nasi, miongoni mwetu
    Tusizidharau tamaduni zao, tuwavumilie
    Pia wapo wengi wa dini mbali mbali, miongoni mwetu
    Tusiwahukumu kwa imani yao, tuwavumilie hivyo
  4. Malezi na mapito yetu sio sawa, miongoni mwetu
    Wengine wameona machungu mengi, tuwavumilie
    Wengine hukasirika haraka sana, miongoni mwetu
    Tusiwe sababu ya machozi yao, tuwavumilie hivyo