Uhuru wa Kweli Lyrics

UHURU WA KWELI

@ Bernard Mukasa

   //utangulizi

   Ninyi mliitwa ndugu muwe watu huru kabisa
   Lakini uhuru huo sio wa kuusingizia
   Isiwe ni sababu - ya kutawaliwa na tamaa hizi
   Tamaa za dunia - msitawaliwe na tamaa za dunia
   Ooh jifunzeni kutumikiana kwa upendo daima
   Kwani sheria ni moja nayo ndiyo upendo

   //kiitikio

Uhuru wangu ee - uhuru wangu
Uhuru wangu wa thamani
Uhuru wangu jamani - uhuru wangu (uhuru)
Unatokana na ukweli

 1. Nikijisifu kwa uongo, nateseka
  Kwani siwezi dhihirisha sifa yenyewe
  Jamii itatarajia kutoka kwangu
  Nisiyoweza kuyatenda, kwani si ya kweli!
 2. Nikifanya udanganyifu, kwenye fedha
  Nikimwona ausikaye ninazizima
  Au nikipokea rushwa, nitanena
  Hata yale yasiyo mema, yanidhalilishe!
 3. Nikikosa uaminifu, kwenye ndoa
  Nitakwepa kuongozana, na mpendwa wangu
  Ili tusije kukutana, na hawara
  Akashindwa kuvumilia, akanipondeza!
 4. Nikizunguka nchi nzima, kuongea
  Uwogo juu ya mwenzangu, najiumiza
  Tukikutana ana njaa, yuko kimya
  Nitadhani wamemwambia, nitapata hofu
 5. Nikimtesa mpwa wangu, nimleaye
  Sitatamani aonane na wazazi wake
  Kwani najua atasema, nimtendeayo
  Na mimi nitadhalilika, nitaaibika!
 6. Nikifanya upendeleo, ofisini
  Kumkweza asiyefaa, najidhihaki
  Jamii ikimhubiri, afaaye
  Nitahisi nakejeliwa na kuunguliwa

  // hitimisho
  ---
  Kwa sababu mimi, ndiye, ninaiandika mwenyewe
  Historia yangu, leo, itakayosomwa milele
  Daima milele, daima milele, daima milele
  Muamuzi wangu ndimi!
Uhuru wa Kweli
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Maria Goretti Mbagala
ALBUMUhuru wa Kweli
CATEGORYTafakari
SOURCETanzania
 • Comments