Maonyo Mbali Mbali Lyrics

MAONYO MBALI MBALI

@ F. E. Nyanza

{ Usitende ovu, usitende ovu,
Jitahidi kukaa mbali na dhambi
Ndugu jihadhari na usitende dhambi mara mbili
Kwani hata kama dhambi moja haitakosa adhabu } *2

{ Usiseme Bwana atatazama sadaka na wingi wa sala
Usiwe (daima) mlegevu katika kusali na kutoa sadaka
Usitunge uongo kwa kuwa hakuna tumaini kwa hilo
Usihesabika pamoja na waovu kwani kumbuka ghadhabu haikawii } * 2

  1. Ujinyenyekeze sana roho yako
    Kwa maana dhabu ya wakosaji ni moto na kufa
  2. Wala usimbadili rafikiyo kwa chochote
    Wala ndugu yako kwa dhahabu ya pili
Maonyo Mbali Mbali
COMPOSERF. E. Nyanza
CATEGORYTafakari
  • Comments