Ahimidiwe Mungu Baba Lyrics

AHIMIDIWE MUNGU BABA

@ John Kasindi

Ahimidiwe Mungu Baba, asiyeyakataa maombi
Maombi yangu, ahimidiwe yeye
Ahimidiwe Mungu Baba asiyeyakataa maombi yangu
Wala hakuniondolea fadhili zake mavumbini
Nami nami siku zote nitaziimba sifa zake zote
Mungu

  1. Mimi nilimlilia Bwana, Mungu kwa sauti
    Sifa zake nikazitangaza, naye amenijibu
  2. Lakini kweli Mungu, Mungu amenisikiliza
    hakika amenisikiliza, maneno ya sala yangu
  3. Enyi mnaomcha Mungu, njooni nyote mkasikilize
    nami nitayasikilizeni, aliyonitendea
Ahimidiwe Mungu Baba
COMPOSERJohn Kasindi
CHOIRKristu Mfalme Kigoma
CATEGORYZaburi
  • Comments