Siri ya Moyo Wangu

Siri ya Moyo Wangu
Performed bySt. Kizito Makuburi
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa
Views9,790

Siri ya Moyo Wangu Lyrics

  1. {Siri ya moyo wangu, ni kilio changu
    Na kilio cha moyo wangu, niione huruma yako } *2
    Mungu wangu kinga yangu, nakuita Bwana
    Ukinigeuka wewe nimekwisha mimi
    Wewe ndiwe fimbo yangu, kimbilio langu
    Ndiwe boma la wokovu, msaada wangu
    Niepushie makucha ya dunia

  2. Kikombe cha uchungu nimekunywa kwa harakwa
    Sasa kimenikwama
    Nimenaswa nimefikwa yamenikuta mimi
    Ee Bwana ninakuita mimi ee Mungu njoo unikamilishe
  3. Najua haina thamani, sala yangu ni chafu
    Ibada haifai
    Nimkimbilie nani zaidi yako wewe
    Naililia huruma yako, mkono wako nishike Bwana
  4. Mimi sistahili kabisa kupokea neema
    Kutoka kwako Bwana
    Ni mchafu ni mdhambi, nimeoza moyoni
    Mikono nakuinulia Bwana, machozi yangu nafukia mimi