Asubuhi Imefika

Asubuhi Imefika
Performed by-
CategoryThanksgiving / Shukrani
Views3,670

Asubuhi Imefika Lyrics

  1. Asubuhi imefika sasa, usiku umeisha, kumeshapambazuka
    Na mchana umewadia, usiku umeisha, kumeshapambazuka
    Ikawa ni asubuhi
    Viumbe,
    Viumbe vyote vishangilie pilka za hapa na pale
    Kwa kuwa Mungu aliye hai ametulinda
    Tushangilie tuimbe, kwa furaha tuimbe
    Kwa kuwa Bwana ni mwema tumwimbie kwa maringo

  2. Nguvu tumejaliwa tumeamka na afya njema
    Mungu ametulinda tumeona siku ya leo
    Hivyo basi tumshukuru Muumba
  3. Nyota zilikuwepo usiku huu wa manene
    Wote tumefumbwa jua tumelala usigizi
    Hivyo basi tumshukuru Mwenyezi