- { Siku zinapita, miaka yapita
Neno lake Bwana halitapita kamwe }*2
- Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini *2
- mmmm mmmm mmm siku hiyo ni ya huzuni mno
mmmm mmmm mmm siku hiyo kweli inatisha
- Kwa maana siku hiyo,
Mavazi yako yatakuwa ni sanda
Kitanda chako kitakuwa jeneza
Na nyumba yako iyakuwa kaburi
Jamaa zako watakutupia udongo,
kwa heri ya milele!
- Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini *2
- { Roho ndiyo roho ndiyo itiayo uzima
Mwili haufai kitu } * 2
- Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini
- Tazameni mimea, shambani
Matunda na maua, vyapendeza
Vyote vitanyauka
Wanyama wa pori, na nyumbani
Na ndege angani, wapendeza
Wote wataangamia
- Ee ndugu sasa utubu rudi
Mrudie Mungu wako
Kwa maana duniani sisi ni wasafiri
Hujui saa na siku ndugu ya kuiacha dunia
Kwa maana duniani sisi ni wasafiri
- Sayari angani zapendeza
Mito na mabonde duniani
Vyote vitatokomea
Mungu ndiye peke ajuaye
Siri ya maisha ya viumbe
Vyake ulimwenguni
- { Siku zinapita, miaka yapita
Neno lake Bwana halitapita kamwe }*2
Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini * 2
|
|
|