Sote Tusimame Lyrics

SOTE TUSIMAME

Sote tusimame kwa heshima ya jina la Bwana
Tumwimbie Mungu wimbo mpya ule wa masifu
Kwa vinanda hata na vinubi tumwimbie
Mungu wetu aliyetuumba, ni Baba wa mababu zetu

  1. Tupige vigelegele, tupigeni na makofi
    Sisi tumekombolewa, tuimbe tushangilie
  2. Kaigeuza bahari, ikawa nchi kavu,
    Njooni tuyasimulie, matendo ya Mungu wetu
  3. Alikemea bahari, mawimbi yakanyamaza
    Mungu wetu ni mkuu, jina lake litukuzwe
Sote Tusimame
CATEGORYEntrance / Mwanzo
  • Comments