Mimi Ndimi Baba Yao Lyrics

MIMI NDIMI BABA YAO

@ Martin M. Munywoki

{Mimi ndimi Baba yao Baba milele (milele),
nao ni wanangu Nitawasikiliza nitasikia (mimi),
wakinililia katika taabu} *2

 1. Mimi ndimi wokovu wa watu, nitawaokoa
  Wakinililia katika taabu yoyote, nitawasikia
  Mimi ndimi aishikaye kweli, nitawahukumu
  Walioonewa na taifa lisilo haki, nitawafungua
 2. Mimi ndimi mchungaji mwe-ema, nitawakusanya
  Waliotawanyikia nchi za ugenini, nitawarejesha
  Mimi ndimi mwa-limu wa watu, nitawafundisha
  Waliolemewa na mizigo yao mizito, nitawapumzisha
 3. Mimi ndimi m-kate wa uzima, nitawashibisha
  Wote wenye njaa na kiu ya haki hakika, nitawashibisha
  Mimi ndimi ufufuo wa kweli, nitawafufua
  Wakinirudia na kutubu maasi yao, nitawasamehe
 4. Mimi ndimi kimbilio la watu, nitawahifadhi
  Waliotengwa kando na jamaa zao, nitawapokea
  Mi-mi ndimi wo-kovu wa watu, nitawaokoa
  Wakinililia katika taabu yoyote, nitawasikia
Mimi Ndimi Baba Yao
COMPOSERMartin M. Munywoki
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYF Major
TIME SIGNATURE6
8
NOTES Open PDF
 • Comments