Nampenda Mungu Muumba Wangu Lyrics

NAMPENDA MUNGU MUUMBA WANGU

@ A. J. Msangule

Nampenda Mungu Muumba wangu, kwa maana amenisikiliza
Amekisikia kilio changu, maombi yangu ameyapokea
{ Nilipokuwa tabuni, Yeye alinishika mkono (tena)
Kifo kiliponisonga, Mungu aliniponya salama } *2

  1. Hatari ya kifo ilinizunguka na vitisho vya mauti
    Vilinivamia nikajawa na mahangaiko ya majonzi
  2. Nikamlilia Mwenyezi Mungu kwa kelele zenye hofu
    Kwa huruma yake akaniponya ee Mungu tegemeo langu
  3. Mungu huwalinda wanyofu wa moyo wasipatwe na mikasa
    Wakikandamizwa huwaokoa maana yeye mwaminifu
Nampenda Mungu Muumba Wangu
COMPOSERA. J. Msangule
CATEGORYZaburi
MUSIC KEYD
TIME SIGNATURE2/4
SOURCEArusha Tanzania
NOTES Open PDF
  • Comments