Palikuwa na Kijana Mmoja Lyrics

PALIKUWA NA KIJANA MMOJA

@ (traditional)

 1. Palikuwa na kijana mmoja jina lake Samweli,
  Alikuwa akimcha Mungu tangu utoto wake

  Alisikia sauti Ikimwita, Samweli, Samweli *2

 2. Alikuwa 'kiitwa na Mungu, lakini hakujua,
  Alikimbilia kwake Eli, Eli hakuelewa
 3. Aliitwa naye Mungu tena, wala hakufahamu,
  Eli 'kashangaa akasema: Mimi sikukuita
 4. Alipoitwa mara ya tatu, Samweli akajibu:
  Nena, Bwana, mtumishi wako anatega sikio.
 5. Mungu akawa pamoja naye, na Israeli nzima
  Ikafahamu kuwa Samweli ndiye nabii wake
Palikuwa na Kijana Mmoja
COMPOSER(traditional)
CATEGORYWatakatifu
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE4
4
 • Comments