Tusali Pamoja

Tusali Pamoja
Alt TitleHe Subiri Niwakumbusheni
Performed bySt. Yuda Thadei Mbeya
AlbumMlipuko wa Sifa
CategoryTafakari
ComposerGasper Idawa
Views4,258

Tusali Pamoja Lyrics

  1. Hee! subiri niwakumbusheni jambo lilo jema wakristu
    Kweli tusikie vyema kwa makini
    Kweli we kijana wewe Baba mama mtuelewe
    Hebu sikia na kutekeleza, hebu sikia na kufanyia kazi
    Kanisa litajengwa kwa familia
    zinazosali pamoja kwa upendo na
    Kukaa kifamilia kushirikishana matatizo yao na kuyatatua

  2. Jumuiya zetu na ibada mbali mbali
    Zimekuwa haswa ni za kina mama
    Jumuiya nyingi zimejaa mama zetu
    Familia gani zilizokosa baba
  3. Jumuiya zetu hazina vijana
    Familia gani zisizo na vijana
    Tumewaachia hasa mama zetu
    Kusali si kwa mama ni familia nzima
  4. Familia yaundwa baba mama na mtoto
    Iweje kusali baba haonekani
    Kama ni motto yule wa mgongoni
    Usiyemuacha peke yake nyumbani
  5. Vijana ni wengi wapo mitaani
    Ukiwafuatafuata wasema wako bize
    Wamemsahau hata Mungu wao
    Siku wanayojua, Jumapili pekee