Nayaweza Yote

Nayaweza Yote
Performed byBMT Ledochowska K/Ndege Dodoma
AlbumMungu
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa
Views4,200

Nayaweza Yote Lyrics

  1. Nalifurahi sana katika Bwana,
    Kwa kuwa mmehuisha fikira zenu
    Najua kudhiliwa na kufanikiwa
    Kwa hali yoyote na kwa mambo yoyote
    Nimefunzwa kushiba na kuona njaa,
    Kuwa na vingi na hata kupungukiwa.
    (Najua) najua kushiba, (najua) na kuona njaa
    (Najua) kuwa navyo vingi, (najua) na kupungukiwa
    (Ni)najua (ni) najua mi

    Nayaweza - Nayaweza mambo yote
    Nayamudu - Nayaweza mambo yote
    Ni katika yeye - Nayaweza mambo yote
    Anipaye nguvu - Nayaweza mambo yote
    Nayaweza - Nayaweza mambo yote

  2. Najua wazi mimi kiumbe dhaifu,
    Ni kwake Bwana maisha yangu nayaweka
    Sina nguvu nje ya mwokozi,
    Ni kwake Bwana maisha yangu nayaweka
  3. Ninaendelea mbele na utumishi -
    Kwani Bwana anitia nguvu -
  4. Nimevipiga vita vilivyo vizuri -
    Na (mwendo) nimemaliza -

    Neema ya Bwana wetu Yesu Kristu,
    Upendo upendo wa Mungu Baba
    Na ushirika wa Roho Mtakatifu (viwe nanyi)
    Viwe nanyi viwe (sasa) sasa (viwe nanyi)
    Sasa hata milele *2