Mungu Awe Nanyi Lyrics

MUNGU AWE NANYI

@ Stanslaus Mujwahuki

{ Mungu awe nanyi, mshirikiane
Mpate amani katika nyumba yenu } *2

 1. Kushirikiana katika furaha,
  Katika uchungu ni matakwa ya Mungu.
 2. Na watoto wenu walee vizuri,
  Wamjue Mungu ndiye muumba wao.
 3. Na matendo yenu yampendeze Mungu,
  Atawajalia uzima wa milele.
 4. Katika uchungu msaidiane,
  Mfarijiane ni matakwa ya Mungu.
 5. Mpatapo shida au matatizo,
  Mumuombe Mungu atawasaidia.
Mungu Awe Nanyi
COMPOSERStanslaus Mujwahuki
CATEGORYHarusi
MUSIC KEYB Sharp Major
TIME SIGNATURE2
4
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments