Pokea Hii Pete

Pokea Hii Pete
Performed by-
CategoryHarusi
ComposerAfred Ossonga
Views4,974

Pokea Hii Pete Lyrics

  1. Pokea hii pete ee mwenzangu,
    Iwe ishara ya pendo langu, na uaminifu wangu kwako

    { Nakupenda hakika, nakupenda ajabu
    Wewe wangu daima mimi wako wewe
    Tutaishi pamoja, tutakula pamoja
    Hadi kifo kifike, kitutenganishe } *2

  2. Jukumu langu ni kukupenda,
    Wakati wa raha na wa shida, na wewe kwangu weka heshima
  3. Safari hii ndefu ya maisha,
    Imeanza leo siogope, tutatembea bila kuchoka
  4. Milima mabonde ya maisha,
    Tutapanda tena tutashuka, tukiwa pamoja siku zote