Asante Mama wa Yesu

Asante Mama wa Yesu
Performed bySt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumAsante Mama wa Yesu
CategoryBikira Maria
ComposerP. F. Mwarabu
Views11,562

Asante Mama wa Yesu Lyrics

  1. Asante Mama wa Yesu, asante sana Mama Maria
    Uliye muombezi wetu, sisi wanao wa dunia
    Baraka za mwana wako, tunazipata kweli Maria
    Yote ni kwa ajili yako, muombezi mwema Maria

  2. Faraja tunazipata, udhaifu unatoweka
    Unyonge unatutoka, imani inaongezeka
  3. Walemavu na wagonjwa, Yesu awafariji sana
    Na pia anawaponya, na kuwaongezea neema
  4. Mapepo wote wabaya, na yule shetani muovu
    Haraka wanakimbia, kwa jina la mwanao Yesu
  5. Uzidi kutuombea, tupate nguvu na uzima
    Tusije tukapotea, tufike mbinguni kwa Baba