Ee Mariamu Wafahamu

Ee Mariamu Wafahamu
Performed by-
CategoryBikira Maria
Composer(traditional)
Views4,351

Ee Mariamu Wafahamu Lyrics

  1. Ee Mariamu wafahamu, wanao wa ugenini
    Tupe, Mama, usalama,
    Utulinde hapa chini, utulinde hapa chini
  2. Nyota nzuri ya bahari, tuliza dhoruba mbaya,
    Na za mwovu, vunja nguvu,
    Simwache kutuogofya, simwache kutuogofya
  3. Na memayo jaza nyoyo, za mayatima waombi
    Utukaze tuongoze,
    Tusichafuke na dhambi, tusichafuke na dhambi
  4. Tukitishwa tukisongwa, na ya mwisho masumbuko
    Uje hima na ujima,
    Kuopoa watoto wako, kuopoa watoto wako
  5. Ukaako wana wako, Maria Mama Bikira,
    Uwinguni kwa amani,
    Waonje furaha bora, waonje furaha bora
Recorded by Glorious Singers Tanzania