Kwa kinywa changu Mungu wangu nitakutukuza,
kwa nyimbo nzuri nitaziimba sifa (zako )
Kwa kuwa Mungu wema wako kwangu mimi ni mkuu siwezi kuelezea
{ Sina kitu Bwana cha kukupa (wewe)
kulingana na mema uloyatenda
Naitoa kwako nafsi yangu (Bwana)
nitendee unavyotaka } *2
- Kama ni pumzi ya uhai umenipa bure,
Sauti nzuri ya kuimbia, yatoka kwako
Nakurudishia sifa na shukrani
- Kama ni elimu, niliyo nayo ni mali yako,
Ujuzi na kazi niliyo nayo vyatoka kwako
Nakurudishia sifa na shukrani
- Magonjwa mengi umeniponya ee Mungu wangu,
Na ajali nyingi umenikinga ee Mungu wangu
Nakurudishia sifa na shukrani
|
|
|