Nani Utamtumikia

Nani Utamtumikia
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumAsifiwe Bwana Mungu (Vol 8)
CategoryTafakari
ComposerGabriel Nghonoli
Views3,818

Nani Utamtumikia Lyrics

  1. {
    Chagueni hivi leo mtakayemtumikia
    Chagua utakayemtumikia ni nani
    Lakini mimi na nyumba yangu, (lakini) mimi (na nyumba yangu)
    lakini mimi na nyumba yangu, nitamtumikia Bwana } *2

  2. Pengine mwenzangu, waitumikia miungu
    Unapopata shida, wakimbilia tunguri,
    Waisahau ahadi yako ya ubatizo
  3. Pengine mwenzangu, waitumikia tamaa
    Maisha yako yote yametekwa na mali
    Waithamini mali badala ya Mungu wako
  4. Mtumikie Mungu, mtegemee siku zote
    Achana na miungu, waganga wa kienyeji
    Kwani Mungu pekee ndiye muweza wa yote