Niruhusu ee Yesu Lyrics

NIRUHUSU EE YESU

@ E. F. Kidaluso

Niruhusu Yesu wangu, niijongee meza yako
Unisamehe dhambi Mwokozi,
uje rohoni mwangu uniokoe
Njoo kaa ndani yangu, nami nikae ndani yako
Ili nipate amani tele, ndani ya Roho yangu nifarijike

{ Wewe Bwana (wewe Bwana wanijua)
Wanijua (hata nafsini mwangu)
Wewe ndiwe tabibu pekee wa roho yangu
Tena ndiwe kimbilio langu }*2

 1. Tazama Yesu wangu ninajongea karamu yako
  Pengine kwako Bwana sikustahili kuijongea
  Unihurumie ee Yesu wangu unisamehe
 2. Hakika kwako Bwana makosa mengi nimeyatenda
  Ubinadamu wangu siwezi kuficha kwako Bwana
  Unihurumie ee Yesu wangu unisamehe
 3. Niwazi Yesu wangu unaujua udhaifu wangu
  Sina chakujitolea mbele yako Ee Yesu wangu
  Unihurumie Ee Yesu wangu unisamehe
Niruhusu ee Yesu
COMPOSERE. F. Kidaluso
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
MUSIC KEYEb
TIME SIGNATURE2
4
SOURCENgokolo Shinyanga
NOTES Open PDF
 • Comments