Uhimidiwe

Uhimidiwe
Performed byBikira Maria Consolata, Bunju
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerAckrey Sissa
Views16,490

Uhimidiwe Lyrics

  1. Nakutumaini wewe Mungu wa huruma
    Naitumaini damu yako ilojaa upendo
    Ninakuhimidi Bwana nakupenda sana
    Ninakuhimidi Bwana Yesu maishani mwangu

    Uhimidiwe - uhimidiwe wewe Bwana uhimidiwe *2
    Unanipenda - uhimidiwe
    Unanijali - uhimidiwe
    Unasamehe - uhimidiwe na kutukuzwa aee

  2. Kila ifikapo kumekucha mimi naamka
    Riziki mtaani Bwana mimi natafuta
    Chochote kila unanipa
    Na hata kama ninakosa
    Tamaa mimi sitokata
    Uhimidiwe ee Bwana Yesu
  3. Tazama na watoto yatima wanakulilia
    Nao mama wajane nao wakusubiria
    Tazama nao wazee
    Tazama nao wafungwa
    Tazama nao wagonjwa
    Uhimidiwe ee Bwana Yesu

    Oo Tuserebuke - tuserebuke tumtangaze ahimidiwe *2
    Tuserebuke kwa shangwe na tuserebuke
    pamoja na tuserebuke ahimidiwe
    Dunia nzima tuserebuke tumtangaze huyoo