Fumbueni Vinywa

Fumbueni Vinywa
Performed by-
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerD. Wasonga
Views2,754

Fumbueni Vinywa Lyrics

  1. { Fumbueni vinywa vyenu (fumbueni) mkapaze sauti zenu
    mkisifu mkishangilia ukuu wa Bwana Mungu wetu
    Mkirukaruka huku mkiimba sifa za Bwana Mungu wetu } *2
    { Pazeni sauti (pazeni sauti) mkiimba kwa furaha
    Fanyeni shangwe kwa zaburi ngoma hata na matari } *2
  2. Tukuzeni sifa zake, tukuzeni sifa zake,
    imbeni imbeni zaburi imbeni zaburi
    Pigeni kelele za shangwe kwa furaha
    Msifuni Mungu wenu kwa kinanda na kinubi
  3. Kwa maana kusifu kwapendeza, kusifu kwapendeza
    Basi njooni tumsifu Bwana Mungu wetu