Hazina ya Mbinguni

Hazina ya Mbinguni
Performed by-
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerD. Wasonga
Views3,763

Hazina ya Mbinguni Lyrics

  1. Hiki ndicho nilichoandaa, siku ya leo
    (Nami) nakusihi ukipokee
    Hii ndiyo shukrani yangu, sehemu ya pato langu
    Itokayo ndani ya mtima wangu

    Hivyo, naileta mikononi mwako (ambapo) nondo hawataiharibu (na kutu)
    Naileta mikononi mwako, ambapo mwizi hawezi kuiba
    naileta mahali salama iwe hazina yangu mbinguni
  2. Ninakutolea moyo wangu wala si mifuko yangu
    Ndiyo kazi ya mikono yangu, nakusihi uibariki
  3. Hata kama ni kidogo nakusihi ukipokee
    Kwani ndicho nilichoandaa kukutolea ee Mungu wangu
  4. Hiki ninachokutolea kikekupendeze Mungu wangu
    Kama ile sadaka ya mtumishi wako, mtumishi wako Abeli