Acheni Kukata Tamaa Lyrics

ACHENI KUKATA TAMAA

@ Bernard Mukasa

{Mwenyezi ameniumba, akanileta kati yenu,
Niwakumbushe watu wake thamani yenu duniani} *2
{Acheni acheni kufa moyo,
Acheni acheni kukata tama
Yeye aliyewaumba anaijua kazi yake } *2

 1. Aliijua siri yenu hata kabla hamjaumbwa,
  Ramani ya maisha yenu, yote imo mikononi mwake
  Magonjwa yanayowatesa na maumivu yasiyokoma,
  Ni madogo kuliko yale aliyoyaponya kwa sekunde
 2. Hali mbaya ya kiuchumi, mlo mmoja madeni mengi
  Ni njia ya kunyenyekea na kumpa Mungu ukuu
  Misiba inayowaliza mnapofiwa na ndugu zenu,
  Ni njia ya wapendwa wenu kwenda mbinguni wakafurahi
 3. Maumivu ya kuonewa kudhulumiwa kusingiziwa
  Ni nafasi ya kusamehe na kujivika utakatifu
  Matatizo ya ndoa zenu na migogoro ya familia,
  Ni bahati mmejaliwa ya kujifunza uvumilivu
 4. Bebeni misalaba yenu, nyamazeni msinung'unike
  Huo ndio wokovu wenu shikilieni msiachie
Acheni Kukata Tamaa
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMMaajabu ya Mungu
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
MUSIC KEYE Major
TIME SIGNATURE3
8
NOTES Open PDF


Hope , Lenti


 • Comments