Amezaliwa Masiya wetu

Amezaliwa Masiya wetu
Choir-
CategoryNoeli (Christmas Carols)
SourceTanzania

Amezaliwa Masiya wetu Lyrics

Amezaliwa Masiha wetu, hoyee hoye hoye
Mwana wa Mungu mkombozi wetu, hoyee hoye hoye
Leo kazaliwa naye Maria na amelazwa
kwenye hori la wanyama, twende tukamwone
Amekuja kwetu mwana wa Mungu kuzichukua
dhambi zetu wanadamu, mkombozi wetu
{ Tumsujudie Bwana Mungu, kwa vigelegele
Tucheze ngoma na kayamba tupige makofi } *2


1. Amelala manyasini, twendeni tukamwone,
Tukamsalimie Mkombozi wetu
Kwa zawadi zetu za dhahabu uvumba na manemane

2. Wachungaji waondoka, waenda Bethlehemu,
Wakamsujudie Bwana Mkombozi,
Wafurahi naye pamoja na Maria naye Yusufu

3. Malaika wamefika wengi na wa mbinguni
Tukajiunge nao tuimbe pamoja utukufu uwe
Kwa Mungu juu amani kwa watu wenye mapenzi mema

4. Tumpokee mkombozi Masiha amekuja
Ewe mtoto Yesu ishi ndani yetu, tuangaze sisi,
Kwa mwanga wako mwanga wa Mbinguni.

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Zaeni Matunda Mema 5814860
Sasa Wakati Umefika 7482439
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442