Login | Register

Sauti za Kuimba

Amin Amin Nawaambia Lyrics

AMIN AMIN NAWAAMBIA

 1. Amin, amin, nawaambia, ninawaambia
  Amin, amin, mmoja wenu, atanisaliti

  Nitampiga mchungaji wa kondoo oo
  Na kondoo wa kundi lake watatawanyika*2

 2. Mwana wa Adamu aenda zake, ilivyoandikwa
  Ole ni wake mtu yule, amsalitiye

  Ole wangu, ole wako, umsalitiye Bwana
  Ingekuwa heri kwetu tusingelizaliwa *2

 3. Twaeni mle mwili wangu, uwe ukumbusho
  Twaeni mnywe damu yangu, iwe ukumbusho

  Nitampiga mchungaji wa kondoo oo
  Na kondoo wa kundi lake watatawanyika*2

 4. Amini, amini na kutubu, enyi mataifa
  Amini, amini na kutubu, turudi kwa Bwana

  Ole wangu, ole wako, umsalitiye Bwana
  Ingekuwa heri kwetu tusingelizaliwa *2

Amin Amin Nawaambia
CHOIR
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
SOURCETanzania
 • Comments