Asante Bwana kwa ukarimu

Asante Bwana kwa ukarimu
Choir-
CategoryThanksgiving / Shukrani

Asante Bwana kwa ukarimu Lyrics

1. Asante Bwana kwa ukarimu wako wa ajabu,
Na fadhili zako hazina mipaka,
Sina budi kusema Bwana asante

Umenijua Bwana kabla sijazaliwa
Maisha yangu umeweka kwenye msitari
Kwa maana umenipenda, umenijali
Nakushukuru ee Bwana asante *22. Ninapotafakari upendo wako kwangu mimi
Na riziki zangu wanipa kila siku
Nashindwa nikulipe nini ee Bwana

3. Na mwili wangu umenipa akili ya kutosha
Kuliko wanyama utashi umenipa
Ufananishwe na nani ee Bwana

4. Uhai wangu umenipa na sasa niko hai
Wengi wamezikwa mimi bado nahema
Nikulipe nini kwa upendo wako

5. Na marafiki ndugu jamaa Bwana umenipa
Dhiki zikinizidi wanifariji
Upendo wako Bwana unanishangaza.

6. Kwa hayo yote siwezi lipa langu shukrani
na mengi bado hata siwezi kusema
Bwana unayotenda kwangu makuu

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442